Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba leo amesema hana mpango
wa kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine katika uchaguzi ujao.
Simba amesema hayo wakati wa mkutano wa wanawake wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Temeke.
Kabla ya mkutano huo yeye pamoja na wajumbe walitembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Temeke na kufanya usafi.
“Leo
wakati tukiadhimisha wiki hii muhimu ya wanawake duniani napenda
kutumia fursa hii adhimu kuwatangazia wanachama wanawake wa CCM kwamba
kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kutogombea nafasi hii ya uenyekiti
taifa katika uchaguzi ujao”,amesema
No comments:
Write comments