Thursday, 2 March 2017

UNENE WAHUSISHWA NA AINA 11 ZA SARATANI

WANASAYANSI wa Uingereza wanasema wamethibitisha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya kunenepa na aina 11 za saratani.
Watafiti wamebaini unene unasababisha saratani kadhaa ikiwemo saratani ya tumbo, ini, matiti, utumbo na mfuko wa kizazi.
Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Imperial jijini London, wanasema, mbali ya kuepuka uvutaji sigara, kutunza uzani unaozingatia afya bora, ni njia muhimu inayopunguza uwezekano wa kuugua saratani.
Shirika la afya duniani linasema asilimia 40 ya watu wazima kote duniani ni wanene

No comments:
Write comments