Thursday, 2 March 2017

MWANAMKE ACHOMWA MOTO KUTEKETEZA MAPEPO

MWANAMKE mkazi wa Managua, amekufa baada ya kufungwa kamba na kurushwa kwenye moto na watu wanaodhaniwa wafuasi wa dhehebu la dini kwa lengo la kuteketeza mapepo.
Watu wa familia yake wameviambia vyombo vya habari kuwa, Vilma Trujillo (25) alishambuliwa na watu wanne wakiongozwa na mtu aliyetajwa kuwa ni mhubiri.
Mhubiri huyo, Juan Rocha amekusha tuhuma za kumuua mwanamke huyo kwa kumchoma moto.
Amedai kuwa, Trujillo amekufa kwa kuwa pepo wabaya walimchukua mwanamke huyo na kumrusha motoni.
Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa ya moto.
Maofisa wa polisi walimkamata Rocha na watu wengine wanaohusishwa na tukio hilo la kumchoma kwa moto Trujilo.
Mume wa mwanamke huyo, Reynaldo Perlata Rodriguez amesema mkewe alichukuliwa na kupelekwa kanisani wiki iliyopita wakati wafuasi wa kanisa hilo walipodai ana mapepo baada ya kujaribu kuwashambulia watu kwa panga.
“Hatuwezi kuwasamehe kwa kile walichotufanyia, alinukuliwa akisema. Walimuua mke wangu mama wa watoto wangu wawili. Nitawaambia nini watoto wangu?” amesema

No comments:
Write comments