Thursday, 2 March 2017

WAZIRI MBARAWA AZINDUA SCANER

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akitilia saini na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing (kulia) ya kukabidhiana scanner mpya ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa scanner mpya ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing.
Muonekano wa Scanner Mpya ambazo zimenunuliwa kwa msaada kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Scanner hizo mpya moja imefungwa katika bandari ya Dar es Salaam na nyingine itafungwa katika bandari ya Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Scanner, mara baada ya kuzindua scanner mpya zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga. 
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:
Write comments