Thursday, 2 March 2017

DC APIGA MARUFUKU ULAJI WA KITIMOTO

Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever na kuwaacha wengine wakiwa hoi.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi mitatu iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi na kusambaa katika kata za Legezamwendo na Mambwe Nkoswe.
Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisema nguruwe wote wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe

No comments:
Write comments