Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa anapoyakumbuka
maisha ya changamoto za miundombinu kwa wananchi wa mikoani
aliyoyashuhudia huonekana mkorofi.
Nape ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ametumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kueleza hisia zake akiweka
picha inayoonesha wananchi wakivuka mfereji mkubwa wa maji machafu kwa
kupita ndani ya maji hayo.
“Niliyashuhudia maisha haya mikoani(38 months), nadhani ndio
nikiyakumbuka naonekana mkorofi!!Iko haja kama Taifa kuangalia
vipaumbele vyetu!” aliandika Nape.
Katika tweet nyingine, Nape aliweka picha ya Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwa amepanda mtumbwi na nyingine
akiwa anashiriki kuvuna mtama na baadhi ya wananchi, na kueleza kuwa
hayo ndiyo yalikuwa maisha ya miezi 38 (miaka mitatu) bila kufafanua
zaidi.
“Haya ndio yalikuwa maisha kwa miezi karibu 38! Big up Cde Kinana,” aliandika.
Nape alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kabla ya kuteuliwa kuwa
Waziri na kuachia nafasi hiyo iliyochukuliwa na Humphrey Polepole.
Tuesday, 18 April 2017
Nape: Nikiyakumbuka Haya… Naonekana Mkorofi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments