Sunday 16 April 2017

RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI YA PASAKA KWA MAKUNDI YASIYOJIWEZA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi zenye thamani  ya Shilingi milioni 11,782,000/= kwa jumla ya vituo 9 katika Mkoa wa Dar es Salaam, 2 Zanzibar na 21 kutoka kwenye mikoa ya Tanzania Bara kwa ajili sikukuu ya Pasaka .
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais, Kamishna wa Ustawi wa jamii, Rabikira Mushi amesema  utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha makundi yenye mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.
Mushi amesema Mikoa mingine iliyofaidika na zawadi hizo ni Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Shinyanga, Morogoro, Kigoma, Ruvuma, Mara, Kagera, Manyara, Tabora, Lindi Mtwara, Singida, Mwanza, na Pwani.
Aidha vitu vilivyofaidika na zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar  ni, Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini, Makao ya Watoto Mburahati, Makao ya Watoto Msimbazi. Makao ya Watoto Kijiji cha Furaha, Makao ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.
Vituo vingine ni Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund, Temeke. Makao ya Watoto Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga, Makazi ya Wazee Wasiojiweza na wenye Ulemavu Nunge Kigamboni.
Kwa upande wa Zanzibar,  Mushi ametaja Vituo vilivyonufaika na zawadi hizo,Kituo cha Watoto Istima – Chakechake, PembaMakazi ya Wazee Wasiojiweza Sebleni – Unguja.
Kwa Mikoa ya Tanzania Bara jumla ya vituo 21 vimefaidika na zawadi ya Rais na baadhi yake ni Mahabusu ya Watoto Moshi, Makazi ya Wazee Wasiojiweza Njoro – Kilimanjaro, Mahabusu ya Watoto Mbeya, Mahabusu ya Watoto Arusha, Mahabusu ya Watoto Tanga, Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzage Tanga, Makazi ya Wazee Wasiojiweza Misufini Tanga.
Hata hivyo, Utoaji wa zawadi  umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Marais tangu awamu ya kwanza makundi haya maalum yamekuwa yakipatiwa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine

No comments:
Write comments