Thursday 6 April 2017

Tanzania, Uganda zasaini ushirikiano sekta ya nishati


SERIKALI ya Tanzania na ya Uganda zimetia saini mikataba miwili kati ya sita ya ushirikiano wa maendeleo katika sekta ya nishati pamoja usafiri wa anga.

Mikataba hiyo imesainiwa jijini hapa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa.

Mojawapo kati ya mkataba hiyo ni uendelezwaji wa mradi wa umeme wa megawati 14 eneo la Kikagati na Morongo ambao kila nchi itapata megawati saba.

Mkataba wa pili ni sekta ya usafiri wa anga ambapo ulisainiwa na Profesa Makame Mbarawa ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.

Akizungumzia makubaliano hayo, Balozi Mahiga alisema Tanzania na Uganda ni nchi marafiki na ndio maana jana wamekubaliana kusaini makubaliano mawili kati ya sita yaliyokuwa awali.

Alisema makubaliano mengine ambayo ni usafiri wa maji, reli, ushirikiano wa Jeshi la Polisi Tanzania na Uganda katika masuala ya usalama, sekta ya utangazaji na mengineyo yatasainiwa kwenye kikao cha wakuu wa nchi kitakachofanyika baadaye mwezi jijini Dar es Salaam.

“Tumesaini makubaliano haya mawili ili kuinua fursa za uchumi kati ya Tanzania na Uganda na huu ni ushirikiano endelevu kwa ajili ya nchi hizi mbili,” alieleza.

Naye Profesa Mbarawa alisema makubaliano hayo yaliyosainiwa jana yatasaidia kuinua fursa za usafirishaji katika sekta ya anga kwani Serikali ya Tanzania mwakani itakuwa na ndege sita za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), hivyo makubaliano hayo yatawezesha ndege hizo kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Uganda.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya ziara ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliyoifanya nchini Tanzania hivi karibuni.

Akizungumzia Watanzania wanane waliokamatwa nchini Malawi, Balozi Mahiga alisema muda wowote kuanzia sasa Watanzania hao wataachiwa kwani awali waliingia nchini humo bila vibali wakati wakijaribu kuingia kinyemela kwenye mgodi wa urani

No comments:
Write comments