Thursday, 4 May 2017

BARUA YA SIMBA YAIUMIZA KICHWA TFF

KATIBU MKUU WA TFF, MWESIGWA CELESTINE


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limethibitisha litatoa barua kwa Simba kuhusiana na suala la pointi tatu za Kagera Sugar, lakini wamelazimika kutulia na kuangalia usahihi wa kuiandika.

Simba imekuwa ikidai barua ya kutaarifiwa kupokwa pointi tatu na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Simba imesema ina barua ya kupewa pointi tatu kutoka kwa TFF kupitia Kamati ya Saa 72, hivyo haitambui kupokwa pointi na inasubiri barua ya kupokwa ili iende Fifa.
Taarifa za ndani kutoka TFF, zimethibitisha TFF imekuwa ikigwaya kutoa barua lakini itaitoa.

“Barua inaandaliwa kwa kuwa ina masuala kadhaa ya kisheria, Simba wavute subira,” Ofisa mmoja wa TFF amesema.

Lakini Ofisa mwingine naye amesema: “Kuna uoga, lazima barua iandaliwe kitaalamu na kisheria maana tayari Simba wameibana TFF.”

No comments:
Write comments