Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo ‘Wapo’
kwaajili ya Rais John Pombe Magufuli iko tayari na inaweza kuachiwa
muda wowote.
Rais Magufuli aliufungulia ‘original version’ ya wimbo huo baada ya
kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na
kumtaka rapa, Nay wa Mitego kuongeza baadhi ya maneno katika wimbo huo
ili uwaguse watu wengi zaidi.
Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo huo iko tayari na ameongeza vitu ngingi ndani ya wimbo huo.
“Kusema kweli wimbo wa Mh Rais umekamilika na muda wowote unaweza
kutoka,” alisema Nay. “Nimeongeza mambo mengi ndani yake, kwahiyo
mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya moto mwingine kwa sababu bado
‘Wopo’ yenyewe inaendelea kufanya vizuri,”
Rapa huyo amedai hawezi kusema ni lini project hiyo itatoka.
No comments:
Write comments