Katibu
wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema hawana wasiwasi
wowote juu ya kuondoka kwa kiungo wao Haruna Niyonzima aliyeenda Simba
kwani huko nyuma wachezaji kibao waliondoka katika timu yao akiwemo
Sunday Manara ‘Computer’ na timu iliendelea kufanya vizuri.
Niyonzima
ameamua kuachana na Yanga kutokana na kushindwana dau la usajili kwani
Simba imemtengea dola 70,000 sawa na Sh milioni 154.8 na mshahara wa
dola 3,000 sawa na Sh milioni 6.6.
Akilimali
amesema Niyonzima aondoke tu Yanga bila wasiwasi wowote kwani ana
uhakika atapatikana mchezaji wa kuziba nafasi yake na timu itafanya
vizuri.
“Mwache
aende tu, Yanga ni timu kubwa na walipita wachezaji wengi zaidi yake
kama vile ‘computer’ na wengine wengi ambao walikuwa wazuri lakini timu
iliendelea kubaki na kufanya vizuri.
“Mwache aende huko alikoenda mchezaji asiye na hisani, Yanga kwanza mchezaji baadaye,” alisema Akilimali.
No comments:
Write comments