Uongozi
wa Yanga umelaani kitendo cha mashabiki wachache wa Yanga kuchoma jezi
namba nane iliyokuwa inavaliwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Wiki
iliyopita, Yanga kupitia Katibu wake Mkuu, Charles Boniface Mkwasa
ilitangaza rasmi kumuachia Niyonzima raia wa Rwanda kuendelea na maisha
yake.
Yanga
ilisema imejitahidi kukaa meza moja na Niyonzima, lakini dau lake
limekuwa kubwa na mwisho wamemuachia aendelee na maisha yake na mwisho
wakamtakia kila la kheri.
Siku
chache baada ya kauli hiyo, ikaonekana baadhi ya mashabiki wakichoma
jezi za kiungo huyo Mnyarwanda wakionyesha hasira zao kutokana na uamuzi
wake wa kuamua kuondoka na kwa kuwa ameanza mazungumzo na Simba.
"Si
sahihi, huwezi kuchoma jezi ya mtu eti kisa kaondoka, Niyonzima si
mchezaji wa kwanza kuondoka au kujiunga na Yanga. Mashabiki wanapaswa
kujitambua na kuelewa mchezo wa soka uko vipi, sisi tunaona hili si
jambo la kiungwana," alisema Mkwasa.
Hata
kabla ya ungozi wa Yanga kutamka kuhusiana na tukio hilo, baadhi ya
mashabiki wa Yanga ambao wengi wanajitambua pia walilaani tukio hilo na
kuliita ni la "kishamba".
usikose habari hii bonyeza hapa kujua kilichojiri HAYA NDIYO YALIYOJIRI JANGWANI BAADA YA NIONZIMA KUTIMKA
usikose habari hii bonyeza hapa kujua kilichojiri HAYA NDIYO YALIYOJIRI JANGWANI BAADA YA NIONZIMA KUTIMKA
No comments:
Write comments