Sunday, 25 June 2017

HANS POPPE ASHINDWA KUVUMILIA ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA


Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe ameibuka na kusema watani wao wa jadi, Yanga salio lao la usajili limekata.

Hans Poppe amesema Simba wamekuwa ni wanaotafuta fedha zao kwa kujichangisha ikiwa ni pamoja na kupangisha maduka au flemu zao pale makao makuu ya Msimbazi.

"Sasa wenzetu walikuwa wanategemea mtu mmoja tu, fedha zinatoka tu na wenyewe wamekaa wanafurahia tu, sasa salio limekata ndiyo maana unaona wana shida," alisema.

Simba imekuwa ikiendelea kufanya usajili huku mambo yakisuasua upande wa Yanga.
usikose habari hii bonyeza hapa kuona ishu nzima UNAYE MPENDA NI NGUMU KUMSAHAU UONGOZI WA YANGA WAFUNGUKA ISHU YA NIONZIMA

No comments:
Write comments