Jumamosi ya June 10 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza game yake ya kwanza ya Kundi L ya kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019 nchini Cameroon dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi.
Katika game hiyo Taifa Stars walilazimishwa sare ya kufungana 1-1, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 27 na baada ya dakika 8 Lesotho wakasawazisha kupitia kwa Thapelo Tale, wakati wa mapumziko na baada ya mechi Samatta alionekana kuwa na hasira kiasi cha kupiga kwa mkono mlango wa kuingilia dressing room.
Baada ya mchezo kama nahodha wa Taifa Stars alilazimika kuongea na waandishi wa habari na swali kubwa lilikuwa kwa nini alionesha kuwa na hasira kiasi kile “Kitu ambacho kimewasaidia Lesotho ni uwanja kuwa mdogo tofauti na Taifa kuhusu hasira mimi sipendagi kushindwa hata sare sijaifurahia kwa sababu tulikuwa tunacheza nyumbani na tulikuwa tunahitaji ushindi kwa lazima”>>> Samatta
“Haikuwa katika akili yangu kupata sare, nafikiri wachezaji wote walikuwa na hasira sio mimi peke yangu labda kwa sababu nilishindwa kujizuia kuiohesha lakini hakuna mtu aliyeyafurahia matokeo”>>> Samatta
Unaweza kutazama video ya makocha wa timu zote mbili na Samatta akijibu kuhusiana na kuonesha hasira

No comments:
Write comments