Kwa
mara ya kwanza, Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe
ametofautiana hadharani kimtazamo na aliyekuwa mshauri wa chama hicho,
Profesa Kitila Mkumbo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
Profesa
Mkumbo na Zitto walitofautiana jana kuhusu Bajeti ya Serikali ya Mwaka
wa Fedha 2017/2018 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Philip Mpango.
Msomi
huyo alikuwa wa kwanza kuandika kwenye akaunti yake ya Twitter
akiimwagia sifa bajeti hiyo pamoja na namna ilivyowasilishwa na Dk.
Mpango, akieleza kuwa ni bajeti safi na kwamba anajivunia kuwa sehemu ya
timu iliyoiwasilisha.
Hata
hivyo, Zitto aliibuka na mawazo kinzani akieleza kuwa bajeti hiyo
haitekelezeki, huku akikumbusha kuwa katika bajeti iliyopita ni asilimia
30 pekee ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo zilitolewa na
kwamba asilimia 20 ya fedha hizo zilipotea.
Jana,
idadi kubwa ya wabunge walionesha kuipokea kwa furaha kuu bajeti
iliyosomwa na Dk. Mpango ambayo pamoja na mambo mengine ilitaja kuondoa
ada ya mwaka ya leseni ya magari, kupunguza kodi ya bidhaa za mazao huku
ikipandisha kodi ya mafuta na bia.
No comments:
Write comments