Mbio za usajili zinaendelea kwa nguvu kubwa, gumzo ni klabu tatu, Simba, Yanga na Singida United, sasa kuhusu kiungo wa Simba, Jonas Mkude kuna habari inayomhusu na ametamka yeye mwenyewe.
Mkude
ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga, ameamua kuweka
wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya kukitumikia
msimu ujao kwa kutoa sharti moja kubwa ambalo ni klabu hiyo kumpatia
shilingi milioni 70.
Mkude
kwa sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya mkataba wake na
Simba kudaiwa kumalizika hivi karibuni, ikiwa ni mwisho wa mkataba wake
wa shilingi milioni 60 aliosaini kuitumikia Simba miaka miwili
iliyopita.
Kiungo
huyo amesema atakuwa tayari kusaini mkataba na Klabu ya Yanga kwa dau
la kuanzia milioni 70 kwenda juu kutokana na kiwango alichonacho kwa
sasa.
“Kwa
upande wangu nipo tayari kutua Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 na
kuendelea hadi shilingi milioni 150 na siwezi kusaini chini ya hapo,
nipo tayari kutua katika timu yoyote kwa kiasi ambacho tutakubaliana kwa
kuwa kiwango changu kipo vizuri.
“Lolote
linaweza kutokea kuanzia sasa, tusubiri kila kitu kitakuwa wazi muda si
mrefu na wadau watajua nitasaini wapi kwa ajili ya msimu ujao, wasiwe
na hofu.
“Mimi
ninachoangalia ni maslahi popote pale watakaofanikiwa kunipa dau ambalo
tutakubaliana, nitakuwa tayari kufanya kazi,” alisema Mkude.
No comments:
Write comments