Thursday 6 July 2017

BAADA YA KUKAA KIMYA KWA MUDA MREFU AMIS TAMBWE AFUNGUKA LIVE ATOA YA MOYONI KUHUSU CHAMA LAKE

Mshambuliaji wa Yanga na timu ya taifa ya Burundi Amis Tambwe amesema katika mechi za michuano ya Ndondo Cup ambazo amezishuhudia hadi sasa, amevutiwa na timu ya Misosi FC yenye maskani yake mitaa ya Tandale.
Tambwe alikutana na shaffihdauda.co.tz kwenye uwanja wa Kinesi na kupiga story kuhusu mashindano ya Ndondo huku akisema, hata Burundi watu wanacheza mechi za mchangani lakini Tanzania hamasa imekuwa kubwa zaidi.
“Nimeshaangalia mechi tatu za Ndondo hadi sasa hivi, mechi yangu ya kwanza kuja kuangalia ilikuwa ya Misosi lakini sikumbuki walicheza na nani. Katika mechi hizo tatu nilizozishuhudia Misosi ndio imenivutia kwa sababu inamashabiki wengi halafu wanacheza mpira mzuri na wana wachezaji wa ligi kuu kama Juma Nyoso.”
“Ni timu nzuri niliona walicheza vizuri na siku hiyo walifanikiwa kushinda magoli matatu, siwezi kuitabilia kufika mbali kwa sababu bado ni mapema kuanzia robo fainali ndio unaweza kuona timu ambayo inaweza ikashinda kombe.”
“Mashabiki wanaokuja uwanjani kuzishangilia timu zao wanatoa motisha kwa wachezaji, wachezaji huwa wanajisikia furaha pale wanaposhangiliwa na mashabiki wao. Vitu kama hivi vipo hata kwetu lakini huku ushangiliaji ni mkubwa kuliko kwetu.”
Juma lililopia Tambwe aliongeza mkataba na Yanga kuendelea kusalia kwa klabu hiyo kwa miaka miwili zaidi.

No comments:
Write comments