Tuesday, 25 July 2017

BEKI MWINGINE WASIMBA ANUKIA SAUZI


Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjale ameanza kurejea katika kiwango chake kutokana na kuwa fiti.

Mwanjale yuko katika kikosi cha Simba kilichoweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya.

Awali, Mwanjale raia wa Zimbabwe alikuwa aachwe lakini baadaye kamati ya usajili ya Simba iliamua kumbakiza.

Beki huyo alitoa msaada mkubwa katika safu ya ulinzi ya Simba hasa mechi za mwanzo wa msimu hadi alipoumia katikati ya msimu.

Uamuzi wa Simba kumbakiza ulichagizwa na kuwa kiungo mzuri wa kuwaunganisha wachezaji na uongozi kwa kuwa ana ushawishi unaotokana na kukubalika na wachezaji wengi.

Lakini uwezo wake wa kucheza pia uliwavutia Simba kwamba anaweza kuwa na mwaka mmoja zaidi wa kucheza na kutoa msaada

No comments:
Write comments