Safari ya kiungo Said Ndemla kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC ya Sweden imewadia.
Hii ni baada ya klabu ya Simba kutoa ruhusa kwa kiungo huyo kwenda kufanya majaribio.
Mwishoni
mwa msimu wa mwaka jana, Simba waligoma Ndemla kwenda kufanya majaribio
AFC ya Sweden ambaye anaichezea Thomas Ulimwengu kwa kuwa walikuwa
wakimhitaji.
Simba walitoa sababu kwamba walikuwa wakimhitaji Ndemla katika mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara pia Kombe la Shirikisho.
Ingawa
uongozi wa Simba umekuwa hautaki kulifafanua suala hilo, taarifa za
uhakika zinaeleza Ndemla ameishapata visa na anaweza kuondoka nchini
wakati wowote kwenda Sweden.
No comments:
Write comments