Roma amesema katika mahojiano na EATV kwamba alijua kuwa atawakwaza baadhi ya watu kwa kutosema na kuweka wazi mambo kadhaa kuhusu tukio hilo ikiwemo kutekwa, walipopelekwa, kilichowatokea wakiwa huko walikopelekwa n.k lakini aliamua kutumia busara na kutosema kitu ili aweze kulinda sanaa na maisha yake kwa ujumla.
“Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka. Ni zaidi ya muziki, japo chanzo ni muziki ndio maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani wala nyumbani. Unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile, tunamaliza pale halafu usiku mwema.”
“Lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea. Labda ningesema ukweli pengine ungekuwa ndio mwisho wa Roma kwenye muziki. Mashabiki wangeshangilia lakini kwa wadau mbalimbali mchango ndio ungekuwa umekwisha,” alisema.
Roma alisisitiza kuwa kama angeweka wazi jambo hilo siku ile ambayo alitoka, ingepelekeaa yeye kuacha muziki na kurudi Tanga kufanya mambo mengine, kwani hakuna mtu ambaye angetaka kuwa karibu naye tena.
“Toka nimetoka mpaka sasa sitaki kutazama video mbalimbali ambazo zinaonesha jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kututafuta. Sitaki kutazama kwa sababu sitaki kukumbuka kabisa hali ambayo nilikuwa nayo kipindi kile. Pia sipendi kabisa kuona mtu mwingine yeyote anakwenda huko chimbo ambako tulikuwa tumewekwa tukipata mateso,” alisema.
Roma na wenzake walitekwa mwezi wa nne mwaka huu walipokuwa katika studio za kutayarisha muziki za Tongwe Records na kupelekwa kusikojulikana kwa muda wa siku tatu na kuja kuonekana wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini
USIACHE KUSOMA NA HABARI HII YA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI NA HALIMA MDEE KWA KUBONYEZA HAPA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI,ALLY HAPI AIBUKA KIVINGINE SAKATA LA HALIMA MDEE
No comments:
Write comments