Hatimaye hofu imepungua katika kikosi cha Yanga baada ya washambulizi wake wawili, Amissi Tambwe na Obrey Chirwa kurejea mazoezini kwa asilimia mia.
Chirwa tayari alianza mazoezi ya taratibu, lakini leo amerejea rasmi na kuanza kujifua na wenzake uwanjani.
Huku Tambwe ambaye alikuwa ameanza mazoezi ya taratibu, gym na na ufukweni, naye amejifua na wenzake leo.
No comments:
Write comments