Friday, 6 October 2017

MUDA MFUPI BAADA YA MANJI KUSHINDA KESI YAKE,HOFU YATANDA JANGWANI JENGO LAKE KUUNGUA


Hofu kwamba jengo la Quality Centre linalomilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji kwamba limeungua, imetanda miongoni mwa wapenda michezo.

Hofu hiyo imetanda baada ya kuwa na taarifa kwamba jengo hilo limeungua muda mchache baada ya Manji kushinda kesi ya tuhuma ya madawa ya kulevya iliyokuwa inamkabiri.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zimeeleza kwamba jengo lililokuwa linafuka moshi huo ni jirani na lilipo hilo la Quality Centre.

“Sisi tuko hapa, inaonekana moshi unatokea nyuma ya Quality Centre,” alieleza mmoja wa mashuhuda.


Tayari katika makundi mbalimbali hasa yale wanaojadili michezo walianza kutoa pole kwa Manji wakiamini mkasa mwingine unamuandama hadi walipoelezwa halikuwa jengo la Quality linafuka moshi huo.

Pamoja na kuwa mfanyabiashara maarufu, Manji amezidi kupaa kwa umaarufu kutokana na kushiriki katika michezo hasa soka.

Hivi karibuni aliamua kujiuzulu uenyekiti wa Yanga jambo ambalo lilionekana ni ahueni kwa Simba huku Yanga wakionekana kutofurahia.

No comments:
Write comments