Ukubwa wa janga la njaa katika Jimbo la Unity nchini Sudan Kusini hali
hii imebainishwa na kitengo cha umoja wa mataifa cha usambazaji misaada
pamoja na familia ambao wameweza kufikiwa.
Wanawake wameweka bayana siku ambazo waliishi kwa wiki kadhaa katika
mabwawa na kwamba wameyanusuru maisha yao kwa kula maua yapatikanayo
kwenye mabwawa na majini, wakati mwingine matunda ya mawese na asali ya
mwituni.
Mwandishi wa BBC alikuwa katika eneo la tukio katikati mwa mji wa Leer ameeleza kwamba watoto wengi wanasumbuliwa na utapiamlo.
Umoja wa mataifa kwa sasa wako kwenye mazungumzo na waasi wa Sudani
Kusini kutoa mwanya wa misaada ya kwanza kufikishwa katika maeneo
wanayoyadhibiti.
Inadaiwa kwamba njaa hiyo ni matokeo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe
ambayo haijawahi kutokea popote ulimwengu imepiganwa kwa miaka sita
mfululizo.
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachojishughulisha na majanga
yasabishwayo na ukame na njaa kimedai kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa
la idadi ya watu walioikimbia Sudan Kusini tangu mwanzoni wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa takribani watu milioni tano wanahitaji
msaada wa chakula haraka sana.Maelfu ya watu walikusanyika kupokea
misaada iliyosambazwa kwa ndege za shirika la chakula duniani mwishoni
mwa wiki.
George Fominyen ni miongoni mwa wafanyakazi , anelezea hali
ilivyokua.''hapa , tulichoona ni watu wengi kufurika na wanasema walikua
hawali vizuri, walikua wakitegemea maji , walikua waiketegemea mizizi
na magugu maji kutoka ziwani na walikula mara moja tu kwa siku. Ni hali
ngumu sana na tuna matumaini kuwa misaada ya kibinadamu itawafikia
wafikia watu hawa''
Sara David anasema kuwa watu wanakufa na njaa''nyumbani hatuna chakula
cha kutosha na kuna vita , tuna matatizo mengi mengi sana nyumbani,
lakini sasa tunahitaji vyakula na tutamaliza matatizo yetu''
No comments:
Write comments