Saturday, 25 February 2017

Anthony Lusekelo amuonya nay wa mitego kufungua kanisa...adai anamchezea mungu kama ana mama amkanye






Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu

Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.“Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili.

"Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara.

"Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” alisema Mzee wa Upako.Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam
majira ya saa 6 usiku mwisho ili kupunguza uhalifu.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema kuwa jeshi hilo limebaini wahalifu wengi hutumia mwanya katika muda huo kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwadhuru waendesha pikipiki.


Aidha, Kamanda Sirro, amesema, kuanzia Februari 18 hadi 23 Jeshi la Polisi Usalama Barabarani limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 460 kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na kukamata pikipiki 1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita katika njia ya mabasi yaendayo haraka huku madereva 27 wakifikishwa mahakamani.


Kuhusu suala la dawa za kulevya, Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mpaka sasa limefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa 257 pamoja na kete za dawa za kulevya 1,526, puli 112 na misokoto ya bangi 247 kutokana na oparesheni inayoendelea.


Alisema baadhi ya watuhumiwa bado awajafikishwa mahakamani kwani upelelezi bado haujakamilika na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili

No comments:
Write comments