AMINI NYAUNGO
Mwanamuziki
na mjasiliamali Jokate Mwegelo ama maarufu kama Kidoti sasa amejaribu
kufungua njia katika michezo, alianza kufungua kiwanja Shule ya
Sekondari Jangwani ambacho mahususi kwa Netball, hii haikuwa kimakosa
bali amedhamiria kuendana na michezo kwani upande wa michezo hauko sawa.
Katika
harakati hizo Jokate ameweza kukutana na mastaa mbalimbali Marekani na
kupiga nao picha huku akisema ”Tupo katika majadiliano leo juu ya
jukumu la wanariadha na watumbuizaji ya kuwa mfano wa kuigwa na kujenga
njia ya kizazi kijacho cha Waafrika” ameandika hayo kupitia ukurasa wake
wa Instagram.
Hii
ni dhahiri kabisa kuwa licha ya kufuatilia mambo yake ya kimaisha
lakini ana tumaini la wazi kabisa kwa ajili ya kulivusha soko letu la
michezo na muziki mbele zaidi.
Kiongozi
anaweza kuangaliwa kwa namna nyingi moja wapo muangalie namna
anavyohangaika kwa ajili ya wenzake , pili angalia namana gani
anajishughulisha, pongezi kwa wote wanaojitolea kwa ajili ya wenzao
No comments:
Write comments