Thursday, 2 March 2017

BEI MPYA YA MAFUTA NI BALAA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei elekezi za mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi Machi mwaka huu ambapo mafuta ya petroli na disel kwa bei za jumla na reja reja imepanda.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Ewura Bw. Titus Kaguo amesema bei hizo zimepanda kutokana na mabadiliko katika soko la dunia ambapo kwa upande wa mafuta ya rejareja, petroli imepanda kwa wastani wa Shilingi 102 kwa lita sawa na asilimia 5.18 huku dizeli ikiwa imepanda kwa shilingi 51 kwa lita sawa na ongezeko la asilimia 2.76.
Bw. Kaguo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi kesho Machi 01, na zitabadilika kulingana na nguvu ya soko katika mkoa husika ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, lita moja ya petroli itauzwa kwa shilingi 2,060 na dizeli Shilingi 1,913 huku kukiwa hakuna mabadiliko yoyote ya bei kwa upande wa mafuta ya taa

No comments:
Write comments