Waziri wa maswala ya kigeni nchini China Wang Yi ameitaka Marekani kuwa makini kuhusu mvutano wake na Korea kaskazini.
''Hali
sio nzuri lakini haifai kulazimishwa kusababisha mzozo'',alisema baada
ya kuwa mwenyeji wa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex
Tillerson.Bw Tillerson alizungumzia kuhusu viwango vya hatari vya mvutano huo siku moja baada ya madai kwamba huenda Marekani ikaishambulia Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini inatengeza silaha ya kinyuklia ambayo inaweza kufika Marekani.
Wiki iliopita nchi hiyo ilizindua makombora ya masafa marefu hatua inayokiuka masharti ya Umoja wa Mataifa.
Bwana Tillerson yuko nchini Beijing katika ziara yake ya mwisho mashariki mwa bara Asia ambayo imetawaliwa na hali ya wasiwasi kuhusu Korea kaskazini.
Nchini Korea Kusini siku ya Ijumaa, alisema kuwa huenda Marekani ikaichukulia hatua Korea kaskazini iwapo itaitisha Korea Kusini ama vikosi vya Marekani.
Rais Donald Trump alichapisha ujumbe wa Twitter akisema Korea Kaskazini inafanya ''tabia mbaya''.
Aliongezea kuwa China ambayo ni ndio mshirika mkuu wa Pyongyang imeshindwa kutoa usaidizi.
Lakini bwana Wang ametetea msimamo wa China akisema kuwa mataifa yote yana jukumu la kutekeleza vikwazo vya UN dhidi ya Pyongyang lakini pia zifanye majadiliano na kutoa utatuzi wa kidiplomasia.
''Tunatumai kwamba pande zote ikiwemo marafiki zetu wa Marekani wataangazia hali iliopo kwa makini ili kufikia uamuzi wenye busara'', alisema Wang.
No comments:
Write comments