Ndege mbili zimegongana zilipokuwa katika anga ya eneo moja la shughuli nyingi za kibiashara huko nchini Canada.
Rubani mmoja amefariki na mwengine kujeruhiwa vibaya. Police wamesema ni miujiza hamna mtu mwingine yeyote aliyejeruhiwa licha ya ndege moja ya hizo kuanguka juu ya paa la mojawapo ya maduka makubwa ya eneo hilo nje kidogo mwa mji wa Montreal.
Ndege nyengine ilianguka eneo la kuegesha magari.
Ndege zote ni za aina ya Cessnas kutoka shule moja ya ufunzi wa urubani - Hali mbaya ya hewa ndio inadhaniwa kusababisha ajali hiyo
No comments:
Write comments