Miezi michache tu baada ya mkongwe wa Muziki wa Afro Pop Bongo, Judith
Wambura ‘Lady Jaydee’ kumtambulisha ‘baby’ wake mpya, raia wa Nigeria
aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Spicy, fununu zinadai kuwa penzi
la wawili hao limefikia tamati. Chanzo chetu kilicho karibu na msanii
huyo aliyefanikiwa kubaki juu kwenye chati kwa miaka mingi, kililiambia
Risasi Mchanganyiko kuwa Jide amekorofishana na mpenzi wake huyo, lakini
sababu hasa za kutokea kwa jambo hilo hazifahamiki.
“Mimi ninamfahamu kwa miaka mingi Jide, ni msiri sana, lakini uzuri wake
ni mtu wa mafumbo, huwa anaongea kwa mafumbo, sasa umeona
alichokiandika Twitter? Nenda kasome ndiyo utaelewa nini ninamaanisha,”
kilisema chanzo hicho.
Risasi Mchanganyiko lilipoifuata akaunti ya Twitter ya mwimbaji huyo
anayetarajia kuzindua albamu yake ya saba mwishoni mwa mwezi huu,
lilikutana na maandiko yaliyosomeka; “Ni kweli niliamua kuondoka,
nikidhani nitapendwa niendako HAKUNA, Nilidhani nitakuta tofauti yoyote
mpaka sasa sijaona.” Chini ya maandishi hayo, mashabiki mbalimbali wa
mwimbaji huyo walikuwa na maoni tofauti, wengine wakisema inaashiria
kuwa mwisho wa penzi hilo, huku wengine wakisema huenda ni mambo yao ya
muziki.
“Jide siyo mtu wa kusemasema mambo yake kirahisi, ana moyo wa peke yake,
ni mtu anayeweza kukaa na kitu moyoni na watu wasijue, unapomuona
anaanza kutupa vijembe kama hivi, ujue kuna jambo, mimi nadhani siku si
nyingi zijazo, kuna mshindo mkubwa utatokea ,” alisema shabiki mmoja.
Mtumwingine aliyechangia katika akaunti hiyo, alimtaka mwimbaji huyo
kuweka wazi juu ya kilichotokea au kinachokuja, kuliko kuanza mafumbo
yanayoweza kuwafanya watu wakazungumza vitu ambavyo kimsingi havipo
kabisa.
“Dada funguka, kama shemela kazingua tuambie, halafu wala usikonde, siku hazigandi,” alisomeka msomaji huyo.
Lakini ili kupataukweli wa tukio hilo, Risasi Mchanganyiko lilifanya
jitihada za makusudi za kumfikia Lady Jaydee, ambaye hata hivyo, simu
yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Meneja wa mwimbaji huyo,
Seven Mosha alipatikana kupitia simu yake ya mkononi na
alipoelezwa kusudi la kupigiwa, aliguna na kuomba muda ili awasiliane na
msanii wake, akiahidi kurejea kwa mwandishi ili kumpa kilichopo.
Dakika kadhaa baadaye, Seven, ambaye pia anamsimamia mkali mwingine wa
Bongo Fleva, Ali Kiba alipiga simu; “Nimeongea na Jide, kwanza amekiri
kweli kile kilichopo Twitter ni chake, yaani aliandika yeye, lakini
kuhusu kama ameachana na Spicy au la, amesema hilo hawezi kuliongelea
kwa sasa, muda muafaka ukifika atazungumza.
Swali: Lakini mashabiki wanasema Jide ni msiri sana na kwa vyovyote kuna
kitu, kwa nini usigusie walau hata kama kuna mzozo, maana haya ni mambo
ya kawaida kwa wapenzi.
No comments:
Write comments