Kinachoendelea kuzungumzwa kila pembe ya nchi ni juu ya tukio
la hivi karibuni la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia
kituo cha Clouds redio na televisheni akiwa na askari wenye silaha
akilazimisha kipindi kinachomhusu Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima
Josephat Gwajima na mama anayedaiwa kuzaa nae kisha kumtelekeza kirushwe
hewani.
Kitendo hicho kimeibua hisia za wengi huku wadau wa habari na watu wa
kada mbalimbali wakilaani vikali kwa vile alichokifanya Rc Makonda ni
kosa la jinai na kuingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Sasa leo Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) kwa pamoja wametoa tamko.
No comments:
Write comments