Kiongozi wa jopo la mawakili waliokuwa wakikitetea Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS), Sinare Zaharani akizungumza na waandishi wa
habari katika Viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam juzi. TLS
ilishtakiwa na baadhi ya wanachama wake wakipinga uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika leo.
By Mussa Juma na Filbert Rweyemamu ,Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Arusha. Hatimaye uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unafanyika leo jijini hapa baada ya kukumbwa na ‘figisufigisu’ za kisiasa na kisheria.
Miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakitishia uchaguzi huo ni kesi mbili zilizofunguliwa Mahakama Kuu na mawakili wawili jijini Dar es Salaam na Dodoma.
Moja ya kesi hizo ilikuwa ikidai kanuni zitakazotumika kwenye uchaguzi huo hazistahili kwa kuwa aliyeziidhinisha hakuwa mtu sahihi, wakati nyingine ilitaka uchaguzi huo ufutwe kwa vile kanuni ni batili.
Kesi hizo zilifunguliwa na mawakili Godfrey Waonga na Onesmo Mpinzile. Lakini zote zilitupwa.
Mkutano wa chama hicho ulianza jana na iliibuliwa hoja ya kumfukuza uanachama Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe.
Hoja hiyo iliibuliwa na mjumbe wa mkutano huo Lawrence Masha alipokuwa akichangia mada zilizowasilishwa na watoa mada, Dk Erick Ng’imaryo na Dk Hawa Sinare.
Dk Mwakyembe alitishia kukifuta chama hicho kama kingeacha misingi yake na kuingiza siasa wakati alipokutaa na uongozi wa TLS mjini Dodoma.
Masha alisema TLS haiwezi kuendelea kuvumilia kuwa na mwanachama ambaye anatishia kuifuta taasisi ambayo yeye ni sehemu yake.
No comments:
Write comments