Saturday, 18 March 2017

Sumbawanga ‘mtambo’ wa kutengeneza radi za kichawi

Ng’ombe waliokufa baada ya kupigwa radi Februari 24, 2015 katika Kijiji cha Kabalenzi wilayani Ngara. Matukio ya radi kuua viumbe wakiwamo binadamu ni ya kawaida katika maeneo mbalimbali duniani. Picha ya mtandao

Sumbawanga. Sumbawanga, kama ilivyo maeneo mengine ya mikoa ya pwani-- Tanga na Pwani (Bagamoyo) na ile ya Kanda ya Ziwa, imekuwa ikisifika sana kwa vitendo vya kishirikina.

Maeneo hayo yababeba sifa ya uchawi, ambazo huenda zikizidiana eneo kutoka eneo moja hadi jingine, huku Sumbawanga ikitajwa kuwa ndiyo ‘iko vizuri’ zaidi kwa uchawi, hasa wa ‘teknolojia’ ya asili ya radi.

Kijiji cha Chipu ndio eneo maarufu kwa sifa ya uchawi wa radi mkoani Rukwa. Chipu ni kijiji kilicho nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga, umbali wa takriban kilometa 30 kutoka Sumbawanga mjini.

Radi za asili zinazodaiwa kutengenezwa katika eneo hilo la ufipa, hudaiwa kutumika kama silaha kwa watovu wa nidhamu.

Mkazi wa Kitongoji cha Katandala mjini hapa, Chela Mwanakatwe ambaye ni mtaalamu wa tiba za asili, anaeleza kuwa zipo aina nyingi za radi kulingana na utengenezaji wake.

Anasema yapo makundi matatu tu ya radi ambayo ni radi ya kuonya ambayo huwa haimdhuru mtu lakini inatokea eneo ambalo yupo mlengwa ili kujenga hisia kwa mtu aliyefanya uasi. Pindi inapotokea baadhi ya watu waliopo eneo hilo, hujiuliza “nani amefanya kosa aende kutubu”.

“Kwa mfano watu wamekaa kwenye nyumba, radi huweza kufika na kufanya uharibifu wa nyumba bila kumdhuru mtu yeyote. Au mpo chini ya mti, radi inafika na kupasua mti pasipo kudhuru mtu,” anasema Mwanakatwe.

Anasema aina ya pili ni radi inayojeruhi ambayo hutumika kumjeruhi yule aliyafanya uasi ili aende kuomba msamaha kutokana na kosa alilofanya. Alisema mara nyingi radi hiyo hutumiwa kwa wale ambao wametenda kosa bila dhamira zao kuwatuma, kushawishiwa na kudanganya.

Anasema aina ya tatu ni radi inayokusudia kuua ambayo mara nyingi mhusika anakuwa amethibitika kutenda kosa na kupewa nafasi ya kuomba radhi, lakini ameshindwa kufanya hivyo. Alisema radi ya aina hiyo haina huruma

No comments:
Write comments