Monday 13 March 2017

Mwanajeshi wa Jordan aliyewaua wasichana 7 wa Israel aachiliwa baada ya miaka 20 jela

Ahmed Daqamseh alitajwa kuwa aliyekuwa na matatizo ya akili

Mwanajeshi wa Jordan ambaye aliwaua wasichana 7 wa shule raia wa Israel ameachilia baada ya kifungo cha miaka 20 jela.
Inaripotiwa kuwa Ahmed Daqamseh, kwa sasa yuko nyumbani kijijini mwao karibu na mji wa Irbid.
Daqamseh aliwafyatulia risasi wasichana wa Israel wakati wa safari yao kwenye kisiwa kilicho karibu na mpaka na Jordan.
Mahakama ya kijeshi ilimtaja kuwa aliyekuwa na matatizo ya akili wakati huo, na kumhukumu kifungo maisha jela
Nchini Jordan hii inamaanisha miaka 25. Hata hivyo baadhi ya watunza sheria wamekuwa wakitaka aachiliwe mapema.
Israel haijasema lolote kuhusu kuachiliwa kwa mwanajeshi huyo.
Baada ya kuwaua wasichana hao, aliyekuwa mfalme wa Jordan aliomba msamaha kwa kisa hicho na kutembelea familia za wasichana hao nchini Israeli kutoa rambi rambi zake.
Jordan pia imelipa fidia.

No comments:
Write comments