Rais wa Korea Kusini aliyetimuliwa mamlakani Park
Geun-hye, ameondoka rasmi katika Ikulu ya Rais mjini Seuol, baada ya
mahakama ya nchi hiyo kumvua wadhfa wa urais kutokana na kashfa ya
kupotea kwa mabilioni ya pesa chini ya utawala wake.
Bi Park alindoka ikuli ambayo inafahamika kama Blue House leo Jumapili, baada ya kuwapa kwaheri wahudumu wake.
Msafara mkubwa ulimsafirisha kuenda nyumbani kwake katika wilaya ya Samseong.
Mamia ya wafuasi wake walikuwa wakimsubiri huko huku karibu polisi 1000 wakitumwa.
Hwang Kyo-ahn, ambaye ni mtiifu kwa Bi Park sasa ndiye kaimu Rais.
Maelfu
ya watu walimiminika barabarani mjini Seoul siku ya Jumamosi
kusherehekea kuondoka kwa Bi Park, huku umati mkubwa wa wafuasi wake nao
ukikusanyika eneo tofauti.
Monday, 13 March 2017
Rais wa Korea Kusini aondoka ikulu baada ya kutimuliwa madarakani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments