Polisi nchini Afrika Kusini wanasema kuwa mtoto mchanga aliyekuwa
ametekwa nyara ndani ya gari la mamake siku ya Ijumaa mjini Durban,
amepatikana akiwa salama
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na uhalifu huo.
Msemaji
wa polisi katika eneo la KwaZulu-Natal Luteni-Kanali Thulani Zwane,
amethibitisha kuwa mtoto huyo alipatikana usiku wa manane kuamkia
Jumapili.
Polisi walikuwa wakifuatilia vidokezo, ambapo baadaye
viliwafanya kumpata ndani ya gari lililokuwa limeegezwa nje ya jumba la
Mariannhill Toll Plaza.
Mtoto huyo wa mwezi mmoja anafahamika kama Siwaphiwe Mbambo.
Tangu
siku ya Ijumaa polisi wamekuwa wakimtafuta mtoto mmoja aliyetoweka,
baada ya gari la familia yao kutekwa nyara katika eneo la Durban.
Kisa
hicho cha utekaji kiliwashtua watu wengi nchini humo na kuwafanya
maelfu ya watu kutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter kutoa
habari aliko mtoto huyo.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja,
Siwaphiwe Mbambo, alikuwa katika kiti cha nyuma cha gari la mamake, pale
gari hilo lilipotekwa na wanaume wawili waliokuwa na silaha nje ya duka
moja kubwa la kununua bidhaa.
Mamake alimnyakuwa mwanawe wa kiume wa miaka minane,
lakini majambazi hao walitoweka kwa kasi na gari hilo, huku mtoto huyo
mchanga Siwaphiwe, akiwa ndani.
Gari hilo lilipatikana baadaye na maafisa wa polisi bila ya mtoto huyo.
Zaidi
ya maafisa 100 wa polisi wamekuwa wakiendesha operesheni kali ya
kumtafuta mtoto huyo, katika kampeini inayoendeshwa na vyombo vya habari
ya mtoto kuibiwa nchini humo.
Watekaji nyara hao waliliendesha gari hilo kwa kasi, huku mtoto huyo mdogo akiwa bado ndani, maafisa wamesema
Sunday 12 March 2017
POLISI AFRIKA KUSINI WAMPATA MTOTO WA MWEZI MMOJA ALIYEPOTEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments