Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Watumia Maji Zigi Juu (Uwamaziju) katika Wilaya Handeni
mkoani Tanga, Phillip Mdoe amesema vijiji 13 vimevamiwa na wachimbaji wa
madini na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akizungumza
kwenye mkutano ulioandaliwa na Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani, Mdoe
amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Ubiri, Sakare, Kwemwewe, Mlesa, Mbomole,
Shebu, Maramba, Amani, Mgambo, Kwemsisi, Shambangeda, Misalai na Kidugo.
Amesema uharibifu umekuwa ukifanyika katika maeneo hayo kiasi cha kuathiri shughuli za kawaida za uhifadhi wa vyanzo hivyo.
Akizungumzia
hali hiyo ya uharibifu wa mazingira, ofisa wa polisi, Michael Joseph
amesema kuna baadhi ya wenyeviti wa Serikali za vijiji vinavyozunguka
vyanzo vya maji wanaodaiwa kushirikiana na wachimbaji kuharibu vyanzo
hivyo.
Joseph amesema jamii inayozunguka maeneo husika inapaswa kuwabana ili wahakikishe kwamba hakuna uharibifu unaoendelea.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaasha Tumbo ametoa siku saba
kwa wenyeviti wa Serikali za vijiji vilivyopo katika Tarafa ya Amani
kuwakamata wanaochimba dhahabu kwenye vyanzo vya maji, vinginevyo
ataagiza wao wakamatwe.
No comments:
Write comments