Rais
wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli ametoa
agizo kwa uongozi wa tanesco kukata umeme kwa Wizara au taasisi yoyote
inayokwepa kulipa bili za umeme.
Mh
Rais ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kuzindua na kuweka jiwe la
msingi katika mradi wa umeme wa msongo wa Kv 132 Mtwara ” Tanesco
pasitokee taasisi ama Wizara hata Ikulu isipolipa umeme we kata tu,
hatuwezi kujiendesha kwa hasara wakati kuna watu wanakwepa kulipia
gharama” wakati serikali inatoa ruzuku zake humu sasa ni wakati Tanesco
ijiendeshe kwa faida.
Aidha Mh Rais
ameonya tanesco kutoingia mikataba ya hovyo na makampuni ya nje
yanayokuja kwa ujanja na alisema kampuni ikitaka kuja kuwekeza umeme
nchini basi waje wazalishe umeme wao na wauze tanesco na wasitegemee
umeme huu kufanya ujanja ili kutorudia mikataba mibovu kama symbion na
makampuni mengine
No comments:
Write comments