Friday, 24 March 2017

Rais Mhe. Dkt. Magufuli avitaka vyombo vya habari kuweka mbele uzalendo.




Rais wa Tanzania Mh Dkt. John Magufuli amevitaka vyombo vya habari nchini kuweka mbele uzalendo kwani wao wana mchango mkubwa katika kuliinua ama kuliangamiza taifa.

Mhe. rais ameyasema hayo alipokuwa akizungumza Ikulu bada ya kupokea hati za utambulisho za mabalozi na kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo waziri mpya wa habari utamaduni sanaa na michezo Mhe. Dkt. Harrisoni Mwakyembe. Rais akasema inashangaza kuwa mataifa ya nje yanathamini na kuheshimu jitihada zinazofanywa na serikali na ndio maana hata rais wa benki ya dunia alikuja nchini kwa mara ya kwanza lakini baadhi ya wananchi hawaoni jitihada hizo, wanabeza.
Kiongozi huyo akawataka viongozi kutovunjika moyo wafanye kazi na wananchi waache kulalamika bila ya kutoa ufumbuzi wa hayo malamiko yao.
Katika hafla hiyo alikuwepo makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassani ambaye alisema kila mtu anapaswa kufanya kazi huku ,kaimu jaji mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwataka viongozi kuzingatia maadili.

No comments:
Write comments