Mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa
awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ameshahojiwa na kamisheni
ya kupambana na dawa za kulevya na kukutwa hana hatia kuhusu tuhuma za
kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya iliyokuwa ikimkabili.
Mbunge huyo wa Jimbo la Chalinze ambaye
pia ni mwanasheria, jina lake lilitajwa kwenye list ya majina 97 ya
watuhumiwa wa biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo RC Makonda
aliikabidhi kwa Kamishna wa kupambana na dawa za kulevya nchini, Rogers
Sianga kwajili ya mahojiano.
Katika taarifa yake aliyoitoa Jumanne hii,
Ridhiwani amesema ameshukuru kuona haki imetendeka katika sakata hilo
lililokuwa likimkabili.
“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali
yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona
ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika
Instagram.
Aliongeza, “Tuunge mkono juhudi hizi.
Tuunge mkono hatua zinazochukuliwa ili kuokoa vijana wetu na kulinda
nguvu kazi ya Taifa #vitadhidiyaMadawa #magufulinikazitu #tanzaniakwanza
#miminikazitu #chalinzenikazitu,”
Alisema hiyo ni taarifa yake ya mwanzo kwa
kuwa amebanwa na majukumu ya kazi na ukifika wakati atoa taarifa rasmi
kuhusu sakata hilo.
No comments:
Write comments