Serikali ya mkoa wa Dodoma imeingia
makubaliano na kampuni ya saruji ya Dangote kuuza saruji katika ujenzi
wa miji mipya ya makao makuu ya nchi (Dodoma).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini
humo mara baada ya kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa kampuni za
Dangote Alhaaj Saada Ladan, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana
amesema kuwa Serikali ya mkoa wa Dodoma imeipa eneo kampuni hiyo ya
Dangote kama eneo la bandari kavu, ambapo saruji inayouzwa nje ya nchi,
zitauziwa kutoka Dodoma.
Alhaaj Ladan kwa upande wake aliishukuru
serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliotoa kwa kampuni hiyo, huku
akisema kuwa ikizingatiwa hata mji wa mkuu wa Nigeria Abuja, ulijengwa
na wataalamu wa kitanzania, na hivyo hawana budi nao kutoa mchango wao
kuijenga Dodoma
No comments:
Write comments