Thursday, 2 March 2017

TUCTA YATOA SIKU 14 KWA SERIKALI KUWARUDISHIA WAFANYAKAZI FEDHA ZA MAKATO YA MIKOPO ZILIZOKATWA KIMAKOSA

Shirikisho  la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limetoa siku 14 kwa Serikali kurejesha fedha za makato ya mikopo ya asilimia 15 zilizokatwa kikamakosa kupitia Bodi ya Mikopo, likisema sera inayotumika imejaa utata.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, alisema  Serikali lazima irekebishe sheria hiyo ya Bodi ya Mikopo kupitia Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi Stadi kutokana na kuwajumuisha wafanyakazi wote katika makato ya asilimia 15 wakati imetungwa hivi karibuni.

Nyamhokya alisema kuwa wakati sheria hiyo inatungwa, baadhi ya wafanyakazi walikwishaingia makubaliano mengine ya kukatwa asilimia 8 katika mishahara yao.

Alisema wamesikitishwa na hatua hiyo ya Serikali, ingawa wanaamini haitalifumbia macho suala hilo.

Aidha Nyamhokya alisema kuna milolongo mingi ya makato katika mishahara ya wafanyakazi ambayo ni zaidi ya asilimia 57, huku pia mazingira ya kufanyia kazi yakiendelea kuwa magumu na Serikali ikishindwa kuongeza mishahara wala kuwapandisha vyeo kwa muda mrefu.

Aidha alisema kwa kawaida mtumishi mwenye mkopo serikalini analipa kwa makubaliano maalumu, lakini mtindo wa bodi hiyo kukusanya fedha za wanufaika kabla ya kuanza kwa sheria husika kumeleta athari kwa watu wengine

No comments:
Write comments