Ujerumani imeiomba Tanzania kuiunga
mkono katika harakati zake za kutafuta nafasi katika Baraza la usalama
la umoja wa mataifa uchaguzi utakaofanyika mapema mwaka 2018.
Ujumbe wa Ujerumani umewasilishwa Tanzania
na mjumbe maalum wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa Rais Dkt
John Magufuli na balozi Harro Adt,na kusema nchi yake inaomba nafasi
hiyo huku ikiwa na agenda nne muhimu.
Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo maalum kutoka Ujerumani
kwa Niaba ya Rais Dkt John Magufuli,Waziri wa mashauri ya kigeni wa
Tanzania Dkt Agustine mahiga amesema wanatambau mchango wa Ujerumani kwa
taifa na afrika kwa Afrika kwa ujumla.Katika kutafuta nafasi hiyo katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa nchi tatu zitakuwa zikiwania nafasi moja huku Isarel na Ujerumani zikipigiwa upatu zaidi.
No comments:
Write comments