Hayo yamebainishwa na Afisa Afya na Mratibu wa Masuala ya Chakula wa
Manispaa ya Temeke Rehema Sadick, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
operesheni hiyo inayoendelea nchini.
“Katika operesheni hii ya kuondoa pombe za viroba tumegundua
wafanyabiashara wengi wanaojihusisha na uuzaji wa pombe kutokuwa na
kibali cha TFDA ambacho hutolewa katika Halmashauri husika,” alifafanua
Rehema Sadick.
Aidha amebainisha kuwa katika msako uliofanyika leo Kigamboni, ambapo
wamekagua zaidi ya maduka matano yanayouza pombe kwa jumla, ni duka moja
tu la Mangale Store lililoko Tuangoma ndilo lililokutwa na kibali cha
TFDA.
Aliongeza kuwa, maduka yote ambayo hayakuwa na vibali hivyo yameamuliwa
kufungwa na kufuatilia vibali katika Halmashauri husika na taarifa za
maduka hayo ikiwemo jina la duka, majina ya mmiliki eneo lilipo pamoja
na namba za mawasiliano vimechukuliwa kwa ajili ya kuchukua hatua.
Afisa Afya huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kuacha kufanya
biashara kwa mazoea na kuhakikisha wanakuwa na vibali vyote muhimu
pamoja na leseni za biashara, kwani kutofanya hivyo ni kukiuka sheria na
kanuni za nchi.
Operesheni ya kuondoa viroba ilianza rasmi Machi 01, 2017 kufuatia agizo
la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kutaka kusitishwa kwa utengenezaji,
usambaaji, uuzaji na utumiaji wa pombe hizo kali maarufu kama
viroba.ifikapo Machi mosi mwaka huu ambapo mpaka sasa operesheni hiyo
imeingia siku ya tano tangua kuanza kwake.
Wednesday 8 March 2017
Wafanyabiashara wasiokuwa na vibali vya TFDA waibuliwa na oparesheni ya viroba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments