Walimu
wakuu wa shule za msingi Magunga na Lubanta, Wilaya ya Mvomero
zilizofanya vibaya kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka jana,
wamekabidhiwa kinyago.
Mkuu wa Wilaya
ya Mvomero, Mohamed Utaly alikabidhi kinyago hicho katika tukio
lililoshuhudiwa na walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu elimu
kata wa wilaya hiyo, shule hizo zitakaa na kinyago hicho kwa kupokezana
ndani ya miezi sita kila shule.
Shule
zilizofanya vizuri zimepatiwa vyeti maalumu vilivyosainiwa na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ili ziongeza bidii.
Ofisa
Elimu ya Msingi wilayani Mvomero, Michael Ligola alisema kutokana na
wilaya hiyo kufanya vibaya kitaaluma katika matokeo ya mwaka jana,
walifanya utafiti mdogo wa kuzunguka kwa baadhi ya kata kuona
kilichosababisha hali hiyo.
Ligola
alisema asilimia 80 ya matatizo waliyoyabaini katika maeneo mengi uwezo
wake upo ndani ya maeneo husika, ikiwamo kuwahusisha wakuu wa shule na
waratibu
No comments:
Write comments