Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika
Machi 8 Mwaka huu, katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana maadhimisho
hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali, na
yataanzia katika Shule ya Msingi Mabatini kuelekea viwanja vya
Mwembeyanga.
Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania
ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.
Kauli
mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga
mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta
Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.
Taarifa
hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za
Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Maadhimisho
hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea
katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi
mbalimbali vya wanawake vitaonesha bidhaa zao.
Aidha,
Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wanakumbushwa kushiriki kwa wingi
katika maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na mikakati ya
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinanazowakabili Wanawake kuanzia
ngazi ya kaya hadi Taifa
No comments:
Write comments