Sunday, 30 April 2017

JPM ASIKILIZA HOJA ZA WANANCHI WA MBOWE


Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli akizungumza katika eneo la Bomang’ombe wakati akijibu hoja za wananchi waliosimamisha msafari wake na kutaka kujua mpango wa serikali katika kufufua kiwanda cha Mashine Tools

Rais Dkt. John Magufuli yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu ambapo amesema Serikali ya Awamu ya tano itafufua viwanda vilivyokufa ikiwemo Kiwanda cha mashine tool kilichopo wilayani Hai.
Akizungumza katika eneo la Bomang’ombe wakati akijibu hoja  za wananchi waliosimamisha msafari wake na kutaka kujua mpango wa serikali katika kufufua kiwanda cha Mashine Tools.
Aizungumzia suala la ukosefu wa umeme katika eneo la Kwasadala, Rais Magufuli amemuangiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki kuhakikisha eneo hilo linakuwa na umeme hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akiwa katika eneo la Maimoria na Majengo Rais Magufuli amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya nchi.
Aidha Rais Magufuli anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa dini mkoani Kilimanjaro pamoja na kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za wafanyakazi Mei Mosi zinazofanyika kitaifa mkoani humo.

No comments:
Write comments