Rais wa Marekani Donald
Trump ametimiza siku mia moja tangu achaguliwe na kuwa Rais wa Marekani
ambapo amefanya maadhimisho kwa kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na
wanahabari katika Ikulu ya White House.
Katika maadhimisho hayo Rais Trump
ametoa hotuba ya kushambulia wanahabari ambapo amelinganisha na
kutofautisha siku mia moja za uongozi wake kuwa ni siku mia moja za
wanahabari kushindwa na kazi yao’, na kutetea mafanikio yake.
Akihutubia umati mkubwa katika jimbo
la Pennsylvania, Rais Trump amesema amekuwa akitimiza ahadi zake kila
siku, hususan kurejesha kazi za viwanda na kumaliza mzozo katika sekta
ya makaa ya mawe.
Aidha, Rais Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao katika dhifa hiyo.
No comments:
Write comments