Manchester United jana huko Stadium of Light wameicaraza Sundrland 3-0 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, na kukalia Nafasi ya 5,kwa matokeo hayo united imewaka rekodi ya kucheza michezo 21 epl pasipo kupoteza mara ya mwisho united kufungwa ni mwezi wa 10 mwaka jana walipopoteza kwa goli 4-0 mbele ya vinara wa ligi hiyo chelsea pale darajani
Hadi Mapimziko, Man United waliongoza 1-0 kwa Bao la Dakika ya 30 la Zlatan Ibrahimovic.
Dakika
ya 43, Sunderland walibaki Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Mchezaji
wao Seb Larsson aliemchezea Rafu mbaya Ander Herrera.
Dakika za 46 na 89 Man United walipiga Bao nyingine 2 kupitia Henrikh Mkhitaryan na Marcus Rashford.
Sasa Man United wameshika Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Man City lakini wao wamecheza Mechi 1 pungufu.
VIKOSI:
Sunderland:Pickford; Jones, Denayer, Kone, Oviedo [Manquillo 39'], Larsson, Rodwell, Cattermole [Borini 66'], N’Dong; Anichebe, Defoe
Akiba: Mannone, Djilobodji, Borini, Pienaar, Khazri, Manquillo, Gibson.
Manchester United:Romero;
Darmian, Bailly, Rojo, Shaw [Blind 61'], Fellaini, Herrera, Pogba;
Lingard [Rashford 64'], Ibrahimovic, Mkhitaryan [Martial 78']
Akiba: Pereira, Tuanzebe, Fosu-Mensah, Blind, Carrick, Martial, Rashford.
Monday, 10 April 2017
MANCHESTER UNITED YA MOURINHO YAWEKA REKODI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments