Katika jitihada za kuhakikisha tatizo hilo linamalizika, Jeshi la
Polisi na Idara ya Uhamiaji limeamua kushirikiana na wananchi kuanzisha
msako mkali ambao umefanikisha kuwakamata wahamiaji haramu 15 kutoka
nchini Ethiopia.
Aidha, Wahamiaji hao walikamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika shamba
la mahindi lililopo katika Kijiji cha Ipumpila Wilaya ya Momba Mkoani
Songwe wakiwa katika harakati za kusafiri kuelekea Afrika ya Kusini.
Hata hivyo, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Elizeus Mshongi amesema
tukio hilo limetokea wakati ambapo tayari raia wengine watano wa
Ethiopia wameshakamatwa na kahukumiwa kwenda jela.
Pia ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni wahamiaji haramu hao
kusaidiwa na Watanzania wanaojua njia za maficho na kuongeza kuwa
watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria.
Sunday 9 April 2017
WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments