Thursday 6 April 2017

Rais Magufuli afanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya


Rais Dkt. John Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Roeland Van De Geerna kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Roeland Van De Geer.
Rais Dkt. John Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Roeland Van De Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka huu.

Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati.

Nae Balozi Roeland Van De Geer amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri na dhamira yake ya kujenga uchumi na kusimamia utawala bora ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa na pia amemuahidi kuwa nchi wanachama wa umoja huo zitaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Tanzania.

Wakati huo huo Rais John Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Yahel Vilan na kumhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na ISRAEL hususani katika masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za kijamii.

Kwa upande wake Balozi Yahel Vilan pamoja na ujumbe wake amemueleza Rais Magufuli kuwa wamefurahishwa na ziara waliyoifanya hapa nchini iliyowawezesha kukutana na viongozi mbalimbali na ameahidi kuwa Serikali ya Israel itajenga jengo la wagonjwa mahututi -ICU katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma kuanzia mwishoni mwa mwaka huu

No comments:
Write comments